Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck ambaye aliwahi kuhudumu kama kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Zambia, amepeleka malalamiko shirikisho la soka duniani (FIFA) akiwa na madai ya malimbikizo ya mishahara na fedha za kuvunja mkataba wake
Sven anaidai Zambia fedha zaidi ya dola 22,000 kutokana na madai hayo ambayo FIFA walidhinisha alipwe
Hata hivyo, Sven amesema bado Zambia haijaanza kumlipa fedha zake na anakusudia kupeleka mrejesho FIFA
Sven alitua Simba miezi michache baada ya mkataba wake kuvunjwa na Zambia baada ya kushindwa kuisaidia timu hiyo kucheza fainali za Afcon 2019 zilizofanyika Misri mwaka uliopita
Sven ana uzoefu wa soka la Kimataifa kwani kabla ya kutua Zambia, alikuwa kocha msaidizi wa Cameroon akiwemo kwenye kikosi kilichotwaa taji la Afcon mwaka 2017