Djuma awazodoa walioponda mfumo wake

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Jan 2018
Djuma awazodoa walioponda mfumo wake
Kocha Msaidizi wa Simba, Mrundi Masoud Juma amesema kwamba, kutokana na ushindi mnono walioupata dhidi ya Singida United, alitaka kuwadhihirishia wale waliokuwa wanamkashifu juu ya mfumo wake mpya anaoutambulisha kwenye kikosi hicho.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Singida walioibuka na ushindi wa mabao 4-0, Juma alisema, watu walitakiwa kuwa na subira kutokana na kile alichokuwa anafanya lakini badala yake walianza kuongea mengi.

Alisema, mfumo wa 3-5-2 unahitaji wachezaji kujituma zaidi na wanapofika kwenye eneo la 18 kushambulia sana, lakini wachezaji walikuwa hawajazoea kutokana na kilikuwa kitu kipya kwao.

"Namshukuru Mungu kwa ushindi wa leo, haikuwa mechi rahisi, Singida ni timu nzuri na kocha wake namuheshimu sana kwa kazi yake, lakini matokeo haya ni kutokana na kutokata tamaa kwani watu waliongea sana juu ya mfumo mpya ndio maana timu ilifanya vibaya Mapinduzi lakini ilitakiwa uvumilivu," alisema Djuma.

Akizungumzia juu ya ujio wa kocha mpya mkuu wa timu hiyo, Mfaransa, Pierre Lechantre aliyekuja na kocha wa mazoezi ya viungo, Mmorocco Mohammed Aymen Hbibi, Juma alisema kwanza anamkaribisha sana na anampa maelezo yote juu ya timu tangu alipoikuta na mabadiliko aliyofanya.

Alisema baada ya hapo iwapo ataamua kuendelea na mfumo wa sasa alioanzisha yeye ni sawa na kama ataamua kubadilisha na kuja na falsafa yake yote kwake ni sawa.

"Mimi sina tatizo kabisa, namkaribisha sana, nitampa maelezo yote ya timu tangu nimekabidhiwa na iwapo akiona inafaa kuendelea na mfumo wa sasa au kubadili na kuleta wake yote kwangu ni sawa," alisema Djuma.

Bin Zubeiry
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’