Tumemisi ushindi wa dakika za majeruhi - Wawa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 Apr 2020
Tumemisi ushindi wa dakika za majeruhi - Wawa

Beki wa Simba Paschal Wawa amesema baada ya kukaa nje kwa mwezi mzima bila ya kushuka dimbani, tayari amekumbuka mikiki mikiki ya ligi kuu

Ligi Kuu ilisimamishwa March 17 baada ya Serikali kusitisha shughuli zote zinazohusisha mikusanyiko katika jitihada ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya COVID-19 nchini

Katazo hilo litaendelea mpaka pale Serikali itakapotangaza vinginevyo

Wawa amesema wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali kwani usalama wa raia ndio jambo muhimu zaidi kuliko kitu kingine

Lakini pia amesema kila mmoja anapaswa kuomba mungu ili janga hilo liweze kumalizika ili maisha yaweze kurejea kama zamani

"Tupo kwenye kipindi kigumu sana lakini tunapaswa kuwa makini na muhimu kwa kila mmoja kuchukua tahadhari na kumuomba Mwenye ez Mungu janga hili limalizike" amesema

Tungependa changamoto hii imalizike salama kwani kama wachezaji tumekumbuka sana majukumu yetu hasa zile purukushani za kusaka matokeo uwanjani, tunaomba mambo yakae sawa ligi irejee"

Ligi ilisimama wakati ambao Simba ilikuwa imebakisha takribani alama 15 iweze kutangaza ubingwa

Katika mechi 10 zilizobaki, Simba inahitaji kushinda mechi tano tu wakiwa kileleni mwa msimamo na alama 71 ambazo ni alama 14 zaidi ya Azam Fc inayofuata nafasi ya pili

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
7h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
13h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
16h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’