Sven ampa tano Ndemla

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 Apr 2020
Sven ampa tano Ndemla

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema timu hiyo bado inahitaji huduma ya kiungo Said Khamisi Ndemla

Sven amebainisha kuvutiwa na uwezo wa Ndemla hasa katika kupiga pasi na umahiri wake katika kupiga mashuti makali

Sven amesema kitu pekee ambacho kinamfanya Ndemla asionekane mara kwa mara uwanjani ni ushindani wa namba huku akibainisha kuwa nyota huyu anahitaji kujifua zaidi ili kuongeza 'fitness'

"Ndemla ni mchezaji mzuri anaetumia mguu wa kulia,anaweza kupiga pasi ndefu zinazofika kwa usahihi,angawa ana changamoto ya kutokuwa na nguvu"

"Tuna idadi kubwa ya wachezaji wanaocheza katika nafasi ya kiungo na anabanwa na uwepo wa wachezaji wenye manufaa makubwa, Kimsingi tuna kikosi kikubwa na tunachoweza kuendelea nacho kwani kila kocha anataka kila eneo liwe na wachezaji bora hivyo wachezaji waliopo wanatosha," amesema Sven

Mkataba wa Ndemla unamalizika mwishoni mwa msimu lakini mwa kauli ya Sven ni wazi nyota huyo atapewa mkataba mpya

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
43m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’