Kocha Mkuu wa Simba, mabingwa wa nchi Sven Vandenbroeck amesema anafahamu kiu ya mashabiki ni kuona timu yao inapata ushindi mnono huku ikicheza kandanda safi
Akiteta na mashabiki kwenye kipindi cha mtandaoni cha ChatNa kinachoendeshwa na idara ya habari na Mawasiliano, Sven amesema anachohitaji ni muda kujenga timu imara itakayokuwa na uhakika wa kuwapa furaha mashabiki
"Nimefahamu mashabiki wa Simba hawapendi timu yao icheze vibaya, lakini pia hawafurahii ushindi mwembamba.. nadhani wanapaswa kuwa wavumilivu tu kwani tulianza kwa kujenga timu baadae kitu kitakuwa sawa"
"Awali nililazimika kutumia mshambuliaji mmoja (Meddie Kagere) kwa sababu hatukuwa na mshambuliaji mwingine zaidi yake, wegine walikuwa majeruhi"
"Baada ya Bocco kupona tulirejesha utaratibu wa kutumia washambuliaji wawili. Tunatengeneza timu ya kushambulia zaidi kwa sababu asilimia 65 ya wachezaji wetu ni washambuliaji," alisema Sven
Ataka ubingwa wa jasho
Katika hatua nyingine Sven amesema anapendelea mamlaka zisubiri changamoto ya ugonjwa wa corona imalizike kisha ligi iendelee
Sven amesema angependa wamalizie mechi 10 zilizobaki, ili watwae ubingwa kwa jasho