Klabu ya Simba msimu ujao imepania kurejea kwa kishindo kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kushindwa kutamba msimu huu
Mabingwa hao wa ligi kuu kwa misimu miwili mfululizo, wanahesabu siku tu kukamilisha hesabu ya ubingwa wa tatu na kama sio corona pengine hesabu hiyo ingekuwa imekamilika
Sasa mpango uliopo ni kuwa kuna maboresho makubwa yatafanywa kwa kikosi ambapo Mtendaji Mkuu wa timu hiyo Senzo Mazingisa amesema wanakwenda kutengeneza kikosi cha maangamizi
Inaelezwa kiasi cha Tsh Bilioni moja zitatumika kukiboresha kikosi cha mabingwa hao wa nchi
Tayari michakato ya usajili imeanza ambapo Simba inafanya usajili wake kitaalamu kwa kuzitumia kampuni za nje kuwafanyia tathmini wachezaji
Senzo amesema usajili wao wa safari hii utazingatia uwezo wa mchezaji pamoja na umri ambapo amesema wanataka kusajili wachezaji ambao wataweza kukaa nao kwa muda mrefu
Amesema mkataba wa chini ambao mchezaji mpya atapewa ni miaka mitatu