Miquissone amuibua Mgossi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
11 Apr 2020
Miquissone amuibua Mgossi

Akiwa ndio kwanza amejiunga na mabingwa wa nchi Simba, kiungo mshambuliaji Luis Miquissone amekuwa gumzo miongoni mwa mashabiki wa Simba

Ni kwa sababu ya mambo makubwa anayofanya tangu alipotua Msimbazi usajili wa dirisha dogo

Mwamba huyo anayetumia jezi namba 11 amefanikiwa kutupia mabao matatu kwenye ligi

Kasi hiyo imemuibua mshambuliaji wa zamani wa Simba Mussa Mgosi ambaye kwa sasa ni kocha wa timu ya Wanawake 'Simba Princess'

Ngosi amesema anajisikia faraja kumuona Miquissone akifanya vizuri huku akiwa ndani ya uzi namba 11 ambao yeye aliutumia wakati akicheza hapo Msimbazi

"Nafurahi kumuona Miquissone anafanya vizuri. Nadhani ni moja ya sajili bora zilizofanywa na Simba msimu huu. Kinachonifurahisha zaidi ni kuona anaitendea haki jezi namba 11 ambayo mimi niliitumia kwa miaka mingi"

Mgosi amesema Miquissone ana nafasi ya kujitengenezea ufalme kunako klabu ya Simba kama hatabweteka na mafanikio alioanza kuyapata mapema

"Asibweteke, na ajiepushe kujiingiza kwenye mambo ambayo yanaweza kumpunguza kasi"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
13h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
19h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’