Simba yakiri kuna changamoto kuwarudisha kina Kagere

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Apr 2020
Simba yakiri kuna changamoto kuwarudisha kina Kagere

Uongozi wa Simba umesema kuwa bado unafanya jitihada kuwarudisha nchini nyota wake raia wa kigeni ambao walirejea makwao kwa ajili ya majukumu ya timu za Taifa

Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema kumekuwa na changamoto kuwarudisha nyota hao kutokana na masharti magumu yaliyowekwa na nchi zao kutokana na janga la corona

Kama ligi itarejeshwa mapema huenda Simba ikaanza kampeni ya kumalizia mechi zilizobaki bila ya nyota hao kwani hata pale watakaporejea nchini watapaswa kukaa karantini kwa siku 14

Nyota ambao wamekwama kwenye nchi zao ni Meddie Kager (Rwanda), Sharaff Shiboub (Sudan), Francis Kahata (Kenya) na Clatous Chama (Zambia)

Rweyemamu amesema wanaendelea kuwasiliana na mamlaka za nchi husika ili kuona jinsi wanaweza kuwarejesha mapema

“Rwanda na Kenya mipaka imefungwa kabisa, hakuna kuingia wala kutoka ndege, unadhani tunaweza kuwasafirisha vipi wachezaji wetu?"

"Hao wa nchi nyingine hata kama wanaruhusiwa kama vile Chama lakini hakuna Shirika la ndege linalofanya kazi zaidi ya Ethiopia, hivyo lazima tusubiri," amesema.

Meneja huyo amesema wachezaji wote wanatakiwa kuendelea kufanya mazoezi na benchi la ufundi lilishapanga program maalum ya kufanya wakiwa nyumbani.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
2h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
7h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
22h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
2d ago
READ MORE β†’