Beki wa kulia wa Simba na timu ya Taifa Shomari Kapombe amesema anafanya mazoezi mara mbili kwa siku ili kuhakikisha anakuwa 'fit' ligi itakaporejea
Ligi imesimama kwa takribani wiki tatu sasa hatma yake ikisubiri maamuzi ya Serikali na mamlaka za usimamizi wa soka kutokana na janga la corona
Beki huyo mahiri amefichua kuwa amejiongezea program ya mazoezi muda wa asubuhi na jioni hufanya program ya mazoezi alioachiwa na wakufunzi wa Simba
Amesema mazoezi hayo yatazidi kumuimarisha na hivyo kuepuka majeraha ambayo yamekuwa yakimsumbua mara kwa mara
"Nimeamua kufanya mazoezi mara mbili kwanza kuujenga mwili wangu kuwa fiti zaidi kutokana na majeruhi ambayo nimekuwa nikikutana nayo huwa yananichukua muda mrefu kupona kwa maana hiyo nikiwa kamili kimwili nitakuwa mbali na matatizo hayo," amesema Kapombe
Kapombe alikuwa miongoni mwa wachezaji walioitwa timu ya Taifa na kocha Etienne Ndayiragije kwa ajili ya michuano ya CHAN lakini michuano hiyo iliahirishwa kutokana na janga la Corona