Mchakato wa Mabadiliko umechelewesha Uwekezaji - Kaduguda

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 Apr 2020
Mchakato wa Mabadiliko umechelewesha Uwekezaji - Kaduguda

Mabingwa wa Soka Tanzania Bara, Simba wamewaomba wadau wote wa soka nchini kuhakikisha wanashirikiana kufanikisha mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji ya klabu hiyo na kuweka historia hapa nchini

Akizungumza jijini jana, Kaimu Mwenyekiti wa Simba, Mwina Kaduguda, alisema kuna changamoto mbalimbali za kiutawala zinazokwamisha kukamilika kwa mchakato huo na hali hiyo inasababishwa na kufuata taratibu za nchi katika kukamilisha mabadiliko hayo.

Kaduguda alisema ili kuhamia katika mfumo huo mpya ambao utaifanya Simba ijiendeshe kisasa, klabu inatakiwa kukamilisha taratibu za mabadiliko hayo kwa wanachama kuridhia vipengele vilivyopendekezwa kwenye katiba ya klabu hiyo.

Kiongozi huyo alisema Simba na wadau wengine wanatakiwa kukamilisha mfumo huo mapema na kamwe kiasi cha fedha cha Sh. bilioni 20 zinazotakiwa kutolewa na mwekezaji, Mohammed Dewji (MO), sio tatizo kwa mfanyabiashara huyo.

"Narudia tena, bilioni 20 sio tatizo kwa Mohammed, isipokuwa tatizo liko kwenye mabadiliko, kutoka katika mfumo wa akina Kaduguda, Kassim Dewji, Hassan Dalali, na kuweka mfumo ambao utatengeneza utaratibu wa kiutawala ili watakapokuja wengine wataufuata na mtu akijaribu kuja na jipya, ataulizwa hiki umekitoa wapi," Kaduguda alisema.

Alisema Simba ndio klabu pekee Afrika Mashariki na Kati ambayo imethubutu kufanya mabadiliko na timu nyingine zinasubiri kuiga endapo vinara hao wa Ligi Kuu Bara watapata mafanikio kwa sababu wengi hupenda kuiga mambo mazuri.

Katibu Mkuu huyo wa zamani wa Chama cha Soka Tanzania (FAT sasa TFF), alisema matarajio ya Simba ni kufika katika hadhi ambayo TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemkorasia ya Congo -( DRC) au Ismailia ya Misri na mafanikio haya yatapelekea klabu nyingine kubadilisha mifumo yao ya uendeshaji.

"Tunataka kuondoka huku kwenye kuendesha mpira kimazoea, Simba inapofanikiwa basi ujue na Yanga pia itafanikiwa, hakuna klabu au mtu anayeweza kuiga kitu kizuri au kisichokuwa na mafanikio, haiwezekani," Kaduguda alisema.

Alisema pia wanachama wa Simba wanatakiwa kutokuwa na hofu na wajumbe waliowachagua wanaunda Bodi ya Wakurugenzi imara ambayo ina malengo ya kuona klabu hiyo inatimiza ndoto zake za kuchukua ubingwa wa Afrika badala ya kufikiria kuifunga Yanga pekee.

"Kwanza kupatikana mimi, Mo amepata mtu sahihi, mimi ninaweza kuwa similiki hata baiskeli, lakini kichwani nina madini ya kutosha, tunaweza kusema Mohammed au Simba ilichelewa kunipata," Kaduguda aliongeza.

Kaduguda alisema pia kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo, ataendelea kukaimu nafasi hiyo mpaka mwaka 2022 baada ya mkutano mkuu uliofanyika Desemba 8, 2019 kuridhia mapendekezo ya Bodi ya Wakurugenzi ambayo ilimteua kuchukua nafasi iliyoachwa na aliyekuwa Mwenyekiti, Swedi Mkwabi.

Naye Ofisa Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, amesema mchakaro wa kubadili mfumo unahitaji muda na haufanyiki haraka kutokana na umuhimu wake katika kufikia malengo.

Aliongeza wakati mfumo bado ukiwa haujakamilika, baadhi ya shughuli za maendeleo kufikia huko zimeshafanyika ikiwamo ujenzi wa viwanja viwili ambavyo zinatumiwa na timu za klabu hiyo.

Nipashe

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
6h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
12h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
15h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’