Wenye uhalali wa kuhoji Bilioni 20 ni Wanasimba - Manara

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 Apr 2020
Wenye uhalali wa kuhoji Bilioni 20 ni Wanasimba - Manara

Afisa Habari na Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesema masuala yanayohusu uwekezaji kwenye klabu hiyo yanawahusu Wanachama na Mashabiki wa Simba

Siku za karibuni baadhi ya vyombo vya habari hasa redio zimekuwa zikiendesha vipindi vya mijadala ambapo moja ya mijadala hiyo ilihoji hatma ya Bilioni 20 ambazo mwekezaji wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' aliahidi kuziweka kwenye akaunti ya mabingwa hao wa nchi baada ya mchakato mzima wa uwekezaji kukamilika

Manara amesema kimsingi wapenzi, wanachama na mashabiki wa Simba ndio wenye uhalali wa kuhoji masuala yanayoihusu klabu yao na sio kila mtu afanye hivyo kwa utashi wake

"Wenye uhalali wa kuhoji kuhusu Bilioni 20 za mwekezaji wa Simba ni mashabiki wenyewe ambao walimpa timu, siyo mtu mwingine tu ambaye hana uhalali," Manara aliiambia EA radio

Mo alishinda zabuni ya uwekezaji kunako klabu ya Simba mwaka 2017 akinunua hisa asilimia 49 kwa kiasi hicho cha fedha

Tangu wakati huo Mo amekuwa ndiye msimamizi mkuu wa klabu ya Simba akilipa mishahara ya wachezaji pamoja na kununua wachezaji wapya

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’