Matola akiri ni ngumu kufuatilia mwenendo wa mazoezi ya wachezaji

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 Apr 2020
Matola akiri ni ngumu kufuatilia mwenendo wa mazoezi ya wachezaji

Kocha Msaidizi wa klabu ya Simba, Selemani Matola, amesema upo ugumu kuwafuatilia wachezaji kwa wakati huu kama wanafanya mazoezi au la katika kipindi hiki ambacho virusi vya Corona vimesitisha shughuli zote za michezo duniani

Corona imesababisha shughuli za soka duniani kote kusimama, ikiwemo Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwa ni agizo la serikali la kusimamisha shughuli zote za kuzuia mikusanyiko lililotolewa mwezi uliopita.

Matola amesema kwa sasa sio rahisi kuwafuatilia wachezaji mmoja mmoja kubaini kama wanafanya mazoezi au la

"Kwa sasa ni ngumu kujua kwamba wachezaji wanafanya mazoezi ama la kutokana na mfumo wa maisha kuwa tofauti na kila mmoja kuwa na mtindo wake mwenyewe", amesema Matola.

"Kinachotakiwa ni kwa kila mchezaji kuwa makini kufanya yale aliyoelekezwa ili awe bora na imara pale ligi itakaporejea", ameongeza kocha huyo ambaye pia aliwahi kuwa mchezaji wa klabu hiyo.

Maoni ya Matola yanaakisi kile kilichosemwa na kocha mkuu wa mabingwa hao wa nchi Sven Vandenbroeck ambaye amependekeza TFF kuvilabu vilabu angalau wiki mbili za kujifua pale ligi itakaporejea

Hatma ya mshikemshike wa ligi kuu kuendelea inasubiri uamuzi wa Serikali kulingana na mwenendo wa maambukizi ya virusi vya Corona

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
6h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
12h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
15h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’