Simba yaipiga 4G Singida United

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Jan 2018
Simba yaipiga 4G Singida United
Vinara wa ligi kuu ya Vodacom Simba leo wametuma salamu kwa timu zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom baada ya kuilaza Singida United mabao 4-0 katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Taifa.

Singida United inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga, Hans van Pluijm ni moja ya timu za kuogofya kwenye ligi kuu ya Vodacom.

Hata hivyo leo walikuwa wepesi mbele ya kikosi cha Simba kilichosakata kabumbu la kitabuni kwelikweli.

Wakati Singida United ikimiliki mpira kwa muda mwingi kwenye kipindi cha kwanza, Simba ilitumia mashambulizi ya kushitukiza kupitia pembeni.



Shiza Kichuya alianza kuifungia Simba bao la kuongoza kwenye dakika ya tatu baada ya kutokea piga nikupige kwenye lango la Singida United kwenye dakika ya tatu.

Bao la pili la Simba lilifungwa na beki Ahsante Kwasi baada ya kuvunja offside na kuwahi pasi murua ya Hamisi Said Ndemla.



Kwenye kipindi cha pili Simba iliendelea kulichachafya lango la Singida United.

Mabadiliko yaliyofanywa na Simba kwenye dakika ya 65 kumuingiza Emanuel Okwi nafasi ya Mzamiru Yassini yaliwanufaisha vinara hao wa ligi kwani Okwi alipachika mabao mawili safi.



La Kwanza alilifunga kwenye dakika ya 65 baada ya kutengenezewa nafasi na Shiza Kichuya huku la pili akiliweka kambani kwenye dakika ya 81 mtengenezaji akiwa Ndemla.

Okwi amefikisha mabao 10 na kuendelea kuwaacha wapinzani wake waliokuwa wamemkaribia baada ya kuwa nje ya dimba tangu mwezi wa 11 mwishoni.



Ushindi huo mujarab unaifanya Simba ijikite kileleni baada ya kufikisha alama 29 na mabao (+23).

Mapema Azam FC ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Majimaji na sasa inabaki nafasi ya pili ikiwa na alama 27.

Mtibwa Sugar iko nafasi ya tatu na alama zake 24 huku Singida United ikibaki nafasi ya nne na alama 23.

Yanga iko nafasi ya tano ikiwa na alama 22, ushindi wa Simba umefungua tofauti ya pointi baina ya timu hizo kuwa saba
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
55m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
18h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
21h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’