Ubingwa haunogi bila ya ligi kumalizika

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 Apr 2020
Ubingwa haunogi bila ya ligi kumalizika

Uongozi wa Simba umesisitiza kuwa lazima ligi imalizike kwa kuchezwa uwanjani na kumpata bingwa halali na sio kumalizwa mapema baada ya kusimama kutokana na sababu ya virusi vya corona.

Tayari klabu kadhaa zilijitokeza na kutaka msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara kumalizwa mapema, kwani hawajui katazo la michezo litamalizika lini kutokana na virusi vya corona.

Kauli hiyo ya Simba imekuja siku chache baada ya baadhi ya viongozi wa timu zinazoshiriki ligi hiyo kutoa maoni ya kuomba ligi hiyo ifutwe licha ya kusalia michezo 10 kumalizika.

Licha ya timu ya Simba kuwa kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa huo kwa mara ya tatu mfululizo wakiwa vinara kwa pointi 71 na kutengeneza utofauti wa pointi 17 na Azam FC, wanashika nafasi ya pili kwa jumla ya pointi 54 bado uongozi wao unaamini ligi imalizikie uwanjani.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingiza amesema kabla ya kuchukua uamuzi lazima kwanza kuangalia hali ya Tanzania na kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya kuhusu ugonjwa huo, ndio nini kifanyike.

"Lazima tuchukue maamuzi tukiangalia hali yetu Tanzania, tuache uongozi kutoka serikalini ufanye kazi yake na kufanya maamuzi kulingana na kile tunachosoma na kuona kinachotokea katika mataifa mengine, lakini ni matakwa yangu ni vema ligi ikamalizika uwanjani, lakini kama ikishindikana basi maisha ni muhimu zaidi kuliko soka,"alisema Mazingiza.

Alisema itakuwa mapema kuamua ligi ifutwe kabla ya mwezi huu na kwa maamuzi ya njia yoyote watakayoenda kutolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Bodi ya Ligi (TPLB), basi yatatakiwa kuzingatia tija na maslahi ya maendeleo ya mchezo huo nchini.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’