Idadi ya wagonjwa wa Corona wafikia 24

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 Apr 2020
Idadi ya wagonjwa wa Corona wafikia 24

Wananchi wameaswa kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Corona ambao umeendelea kusababisha hofu kwa maisha ya watu kote duniani

Jana Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alitangaza uwepo wa wagonjwa wengine wapya wanne wa maambukizi ya virusi vya coronahapa nchini

Katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari mapema jana, kati ya wagonjwa hao wanne, wawili wanatoka Tanzania Bara na wawili wanatoka Zanzibar

β€œWizara ya Afya imethibitisha kuwepo kwa kesi mpya nne za maambukizi ya virusi vya corona (COVI-19) zilizopatikana Dar es Salaam, Mwanza na Zanzibar na kufanya kuwepo kwa jumla ya kesi 24 zilizoripotiwa tangu kuanza kwa ugonjwa huu nchini,”  ilisema sehemu ya taarifa hiyo

Serikali imetoa msisitizo kwa Wananchi kusikiliza maelezo ya wataalamu wa Afya kujikinga na maambukizi ya virusi vya COVID-19 hususan kwa kunawa mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka

Aidha, Wananchi wamesisitiziwa kuzingatia maelezo mengine yanayohusu kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima na kukaa umbali usiopungua mita moja kati ya mtu na mtu

Β 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
11h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
14h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’