Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) kupitia ukurasa wake wa mtandao Instagram limeweka kumbukumbu muhimu inayowahusisha mabingwa wa nchi Simba kwenye michuano ya ligi ya mabingwa
Ilikuwa mwaka 1979 walipoiondosha Mufulira Wonderers kwenye michuano ligi ya mabingwa kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-4
Utamu wa kumbukumbu hiyo unatokana na Simba kupata ushindi wa mabao 5-0 ugenini ikiwa imefungwa mabao 4-0 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam
Ni tukio la kihistoria ambalo CAF wameliweka kama kumbukumbu muhimu kwenye mtandao wao
ADVERTISE HERE