Inaelezwa uongozi wa Simba umepania kwelikweli kuinasa saini ya mshambuliaji wa zamani wa Azam Fc Kipre Tchetche anayechezea Kedah Fc ya huo Malaysia
Nyota huyo mwenye rekodi nzuri ya kuzifumania nyavu, anaweza kurejea nchini kama mabosi wa Simba watafikia makubaliano na klabu yake ya Kedah Fc ambayo alijiunga nayo mwezi Disemba mwaka uliopita
Kulingana na taarifa ya gazeti moja la kila siku nchini, Tchetche ameweka mezani ofa ya mshahara wa Tsh Milioni 20 huku dau la usajili likitajwa kufikia Tsh Milioni 680
Hata hivyo uongozi wa Simba pengine utahitaji kujiridhisha na uwezo wa nyota huyo ambaye kwa miaka takribani mitano sasa amekuwa nje ya Tanzania
Wakati akiwa klabu ya Azam Fc Tchetche ndiye aliyekuwa mshambuliaji kiongozi wa timu hiyo akishirikiana na nahodha wake John Bocco ambaye kwa sasa ni nahodha wa Simba
Katika kikosi chao kilichotwaa ubingwa msimu wa 2013/14 bila ya kupoteza mchezo, beki Paschal Wawa ndiye aliyekuwa kiongozi wa safu ya ulinzi