Simba yajipanga kuwarejesha wachezaji wake walio nje ya nchi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
6 Apr 2020
Simba yajipanga kuwarejesha wachezaji wake walio nje ya nchi

Uongozi wa klabu ya Simba unaandaa utaratibu wa kuwarejesha nchini wachezaji wake ambao wako nje ya nchi

Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amesema baadhi ya nyota wa kigeni wa timu hiyo walipewa ruhusa kurejea kwenye nchi zao kujiunga na timu za Taifa

Lakini kutokana na janga la Corona, baadhi ya nchi zimefunga mipaka yake na kuzuia safari kutoka kwenye nchi hizo hivyo kuwaweka nyota hao kwenye wakati mgumu

"Wachezaji wetu waliosafiri nje ya Tanzania, kabla ya mechi zetu mbili dhidi ya Azam na Yanga, tulipokea barua za wachezaji kuhitajika na timu zao za taifa kwa ajili ya kufuzu michuano ya AFCON. Tulipokea barua kutoka Kenya, Zambia, Rwanda, Msumbiji, Sudan na kama tungewazuia tungeadhibiwa na FIFA," amesema Senzo

"Wakati tunawaruhusu, serikali ya Tanzania ilikuwa bado haijatoa maamuzi juu ya janga la Corona kuwa wageni wakifika lazima waingie karantini kwa hiyo kwa sasa tunaangalia njia gani wataweza kurudi kwa wakati wakae karantini halafu wajiunge na timu"

Wachezaji ambao wako nje ya nchi ni Meddie Kagere (Rwanda), Francis Kahata (Kenya), Luis Miquissone (Msumbiji) na Sharaff Shiboub (Sudan)

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
8h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
11h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’