Kutua Simba fresh tu - Mwamnyeto

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 Apr 2020
Kutua Simba fresh tu - Mwamnyeto

Beki na nahodha wa Coastal Union, Bakari Mwamnyeto amefungukia usajili wake wa kutua Simba ambapo kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na timu hiyo.

Tangu usajili wa dirisha dogo uliofungwa Januari 15, mwaka huu, beki huyo ilielezwa kuwa, amesaini mkataba wa awali wa kuitumikia Simba, akisubiri msimu uishe ajiunge na timu hiyo.

Baada ya tetesi kuwa nyingi, hivi karibuni taarifa mpya zilitoka kwamba, tayari Simba imetoa gari na kiasi cha Sh milioni 85 kumchukua beki huyo, huku mwenyewe akiwa bado hajazungumza chochote juu ya usajili wake huo.

Alipotafutwa beki huyo mahiri na tegemeo wa Coastal alikiri kuwa Simba wamemfuata wakitaka kumsajili lakini bado kuna vitu havijakamilika, hivyo wakifikia muafaka basi anamwaga wino Msimbazi.

"Ni kweli Simba wamenifuata na kuhitaji huduma yangu, mimi nipo tayari kwenda Simba kama tutafikia muafaka mzuri na kutimiza mahitaji yangu kwa sababu mpira mimi ndiyo kazi yangu kwa hiyo naweza nikacheza popote pale, siyo Simba pekee," alisema Mwamnyeto.

GPL

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
41m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’