Inaelezwa uongozi wa klabu ya Simba umeanza jitihada za kuinasa saini ya mshambuliaji wake wa zamani Emmanuel Okwi
Okwi aliondoka Simba mwishoni mwa msimu uliopita baada ya mkataba wake kumalizika akijiunga na klabu ya Al Ittihad Alexandria ya Misri
Okwi alisaini mkataba wa mwaka mmoja ambao unamalizika mwishoni mwa msimu
Tangu Okwi aondoke Simba, mabingwa hao wa nchi wamekosa mchezaji wa aina yake na hivyo wanaweza kumrejesha kuimarisha kikosi chao ambacho kitashiriki michuano ya ligi ya mabingwa
Hata hivyo Simba italazimika kuandaa dau nono kuweza kumnasa kwani moja ya sababu iliyomfanya aondoke ni baada ya Simba kugomea ofa aliyokuwa akiitaka
Inaelezwa Okwi alitaka dau la zaidi Tsh Milioni 100, mshahara wa Tsh Milioni 15 lakini mkataba wa mwaka mmoja