Benchi lamkera Shiboub

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 Apr 2020
Benchi lamkera Shiboub

Kiungo fundi wa Simba Sharaff Elden Shiboub raia wa Sudan alianza maisha vyema kunako mabingwa hao wa nchi

Wakati wa kocha Patrick Aussems, Shiboub alijihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza

Lakini tangu timu hiyo ikabidhiwe kwa Sven Vandenbroeck, fundi huyo wa mpira amepoteza nafasi kwenye kikosi cha kwanza

Shiboub amekuwa na nafasi finyu ya kucheza na wakati mwingine huwa anakosekana hata kwenye orodha ya wachezaji wa akiba

Pamoja na ushindani mkubwa wa namba kwenye kikosi cha Simba, lakini Msudan huyo anaamini anastahili kupewa nafasi

Inaelezwa Shiboub ni miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao iko ukingoni lakini anasuasua kuongeza mkataba mwingine

Klabu ya El Hilal aliyokuwa akiitumikia imeingia kwenye vita ya kumuwania nyota huyo ambaye ni tegemeo kwa timu ya Taifa ya Sudan

Pia inaelezwa Shiboub ana ofa kutoka nchi za Misri na Afrika Kusini

Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amesema Shiboub ni miongoni mwa wachezaji ambao wako kwenye mchakato wa kuwaongeza mkataba na hawana mpango wa kumuacha

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
6h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
12h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
15h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’