Aussems amtaja Mkude mafanikio ya Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 Apr 2020
Aussems amtaja Mkude mafanikio ya Simba

Aliyewahi Kocha wa Simba SC, Patrick Aussems amemtaja Jonas Mkude kuwa ni miongoni mwa wachezaji muhimu ambao waliifanya timu hiyo kufanya vizuri katika michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2018/19.

Simba ikiwa chini ya kocha huyo raia wa Ubelgiji alifika hadi hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo waliondolewa kwa kufungwa jumla ya mabao 4-1 na miamba ya soka la DR Congo TP Mazembe.

Aussems ambaye alimtakia siku njema ya kuzaliwa Mkude siku mbili zilizopita, alimzungumzia kiungo huyo kwa kusema aliifanya Simba kuwa na nguvu katika eneo la kiungo kwa kushirikiana na James Kotei ambaye kwa sasa anacheza soka la kulipwa Belarus.

"Jonas ni mchezaji mzuri mwenye uwezo wa kuifanya timu kucheza kuanzia nyuma, alikuwa akifanya kazi kubwa na Kotei, nilikuwa nikiona tupo salama wakicheza pamoja, kuna muda yalikuwa yakitokea makosa ya kiuchezaji lakini ndio soka lilivyo," alisema kocha huyo.

Aussems ambaye bado yuko kwao akisaka mchongo mpya, alifutwa kazi katika mazingira ya kutatanisha huku akiwa kipenzi cha mashabiki wa Simba.

Kocha huyo ameingia kwenye historia ya klabu ya Simba baada ya kuwawezesha mabingwa hao wa nchi kucheza robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
56m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’