Hatma ya Ligi mikononi mwa kamati ya Utendaji TFF

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 Apr 2020
Hatma ya Ligi mikononi mwa kamati ya Utendaji TFF

Wakati hatma ya ligi kuu ikiendelea ikisubiri majaaliwa ya hali ya maambukizi ya Corona, wasiwasi umeanza kuibuka kuwa msimu unaweza usifike mwisho

Serikali ilisimamisha shughuli zote za michezo kwa muda wa siku 30 baada ya janga hilo kuingia nchini

Hata hivyo idadi ya maambukizi imeendelea kuongezeka huku Serikali ikiendelea kuchukua tahadhari kulinda usalama wa wananchi wake

Awali ligi ilitarajiwa kurejea mwezi huu lakini uamuzi huo utategemea na kauli ya Serikali pamoja na kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF

Tayari TFF imetangaza kusogeza mbele tarahe ya kumalizika kwa ligi kutoka May 30 mpaka Juni 30

Kulingana na taarifa iliyotolewa na TFF juzi, Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo itafanya maamuzi ya mwisho kama ligi haitarejea ifikapo mwezi Juni

Changamoto ya Corona imeendelea kusitisha shughuli zote za michezo kwa karibu mataifa yote duniani

Nchi ya Ubelgiji imekuwa ya kwanza kutangaza kumaliza msimu bila ya ligi kumalizika huku klabu ya Brugge iliyokuwa ikiongoza ligi kupewa ubingwa

Mamlaka za soka nchini humo zilitangaza uamuzi huo jana huku wakitangaza kuwa hakuna timu ambazo zitashuka daraja

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
18h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
21h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’