Simba kufanya kweli uwanja wa Taifa leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Jan 2018
Simba kufanya kweli uwanja wa Taifa leo
Leo kikosi cha Simba kitashuka katika dimba la Taifa kumenyana na Singida United kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 13.

Mchezo huo ni muhimu kwa Simba kupata ushindi ili kuendelea kujiimarisha kileleni wa msimamo wa ligi na kuongeza tofauti ya pointi baina yake na mahasimu wake Yanga waliolazimishwa suluhu ya bila kufungana na Mwadui FC jana.

Simba itashuka katika dimba la Taifa ikiwa na shauku moja tu, kutuliza mzuka wa mashabiki wake ambao hawana furaha baada ya timu hiyo 'kuboronga' kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi sambamba na kutupwa nje kwenye michuano ya kombe la FA (ASFC).

Mshambuliaji Emanuel Okwi ambaye ndiye kinara wa upachikaji mabao ligi kuu ya Vodacom anatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji ya Simba.

Okwi alitua kambini juzi mkoani Morogoro na jana kusafiri na kikosi cha Simba kurejea jijini Dar es salaam.

Mashabiki wa Simba wameaswa kufurika kwa wingi kwenye dimba la Taifa ili kuipa sapoti timu yao.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’