Corona yaua mamia Afrika

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Apr 2020
Corona yaua mamia Afrika

Kulingana na BBC, Kituo cha udhibiti na kuzuia magonjwa vya Umoja wa Afrika kimesema kuwa watu 173 wamepoteza maisha baada ya kuambukizwa virusi vya Covid-19 barani Afrika.

Ugonjwa wa corona umeenea katika nchi 50 barani. Kwa ujumla, watu 5,413 wameambukizwa.

Mpaka sasa hakuna taarifa zozote za maambukizi nchini Lesotho, Sudani Kusini, visiwa vya Sao Tome na Principe, comoro na Malawi.

Hapo jana eneo lililojitangazia uhuru wake Somaliland lilithibitisha kuwepo na maambukizi ya watu wawili.

Redio Kulmiye imesema mmoja kati ya walioambukizwa ni raia wa China aliyekuwa akiishi katika mji wa Berbera. Mwingine ni raia wa Somalia ambaye hivi karibuni alirejea kutoka nchini Uingereza.

Somaliland imesambaza vikosi vyake mitaani na kupiga marufuku utafunaji wa mirungi mitaani kuepuka kusambaa kwa virusi.

Afrika Kusini ina idadi kubwa ya maambukizi,ikiwa imefikia 1,353, watu saba wakiwa wamepoteza maisha.

Watu 11 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya corona tangu jana nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo na kufanya idadi ya walioambukizwa kufikia 109 na vifo vinane.

Wagonjwa wa tatu hadi sasa wameripotiwa kupona lakini mgojwa wa kwanza hadi sasa yungali hospitalini , serikali haijamruhusu kurejea nyumbani kwake.

Kwa Tanzania, Serikali imethibitisha kifo cha mtu mmoja aliyekuwa na maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo

Mpaka sasa watu 19 wameambukizwa huku mamia wakiwekwa kwenye karantini kwenye maeneo mbalimbali

Tuendelee kuchukua tahadhari kuepuka maambukizi ya virusi hivyo hatari

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
35m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
18h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’