AFCON imenipa heshima, bado kombe la dunia - Manula

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Apr 2020
AFCON imenipa heshima, bado kombe la dunia - Manula

Mlinda lango namba moja wa Simba na timu ya Taifa, Aishi Manula amesema ni wachezaji wachache ambao katika maisha yao ya soka hupata nafasi ya kushiriki michuano mikubwa kama AFCON

Manula amesema nafasi aliyoipata kushiriki michuano hiyo mwaka uliopita ni heshima kubwa kwake

Amesema fainali hizo zilizofanyika mwaka uliopita nchini Misri zimeongeza thamani kwenye maisha yake ya soka, hivyo anajivunia na sasa atamani kushiriki Kombe la Dunia na kikosi cha timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’.

"Kupitia Afcon uzoefu niliopata natamani kushiriki fainali za Kombe la Dunia na timu ya taifa na inawezekana kama mipango itakaa sawa, kila mchezaji anatamani kushiriki michuano mbalimbali katika maisha yake ya soka" amesema

Manula ni miongoni mwa wachezaji 23 waliounda kikosi kilichocheza Fainali za Mataifa ya Afrika baada ya miaka 39 bila kushiriki michuano hiyo mikubwa Afrika ambayo pia timu hiyo ilifanya vibaya kwani iliondolewa katika hatua za makundi.

Aidha kipa bira huyo kwa misimu mitatu mfululizo ligi kuu ya Tanzania bara, amesema mafanikio yanayopatikana ndani ya Simba yanatokana na muunganiko mzuri kuanzia kipa kwa kushirikiana na wachezaji wengine wanaunda kikosi hicho.

Pia alimpongeza kocha wa makipa wa timu yao, Muharami Mohamed, kwani amekuwa msaada mkubwa na anawapa nafasi ya kutoa maoni kwa makosa yanayojitokeza kwenye michezo wanayocheza

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’