Sven anawatamani kwelikweli Yanga

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
30 Mar 2020
Sven anawatamani kwelikweli Yanga

Ukweli ni kwamba mpaka leo Mkufunzi wa Simba Sven Vandenbroeck bado haamini kama timu yake ilishindwa kuibuka na ushindi kwenye mechi zote mbili za Ligi dhidi ya Yanga msimu huu

Sven aliyeanza majukumu ya kuinoa Simba mwezi Disemba 2019, aliwaongoza mabingwa hao wa nchi kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Yanga uliopigwa Januari 04 2020 akishuhudia timu yake ikipoteza uongozi wa mabao mawili na kulazimishwa sare ya 2-2

Lakini pia Machi 08 akaishuhudia timu yake ikipoteza mchezo kwa kufungwa bao 1-0 katika mchezo ambao Simba ilitengeneza nafasi nyingi na kutawala mchezo kwa muda mwingi

Pamoja na timu yake kujihakikishia ubingwa wa tatu mfululizo, Sven amesema anatamani apate nafasi nyingine ya kucheza na Yanga kwenye michuano ya kombe la FA

"Ukifuatilia mechi zote mbili tulizocheza nao, tulikuwa bora zaidi nayo na inakuwa ngumu sana kuamini kuwa tulishindwa kupata matokeo. Nadhani jambo pekee ambalo walikuwa nalo kwenye mechi zile ni bahati," alisema Sven ambaye yuko mapumziko baada ya ligi kusimama kutokana na janga la virusi vya Corona

"Wakati mwingine matokeo yasiyotarajiwa hutokea.. Kikosi changu kiko tayari kucheza nao kwa mara nyingine hasa ikitokea tumekutana kwenye michuano ya kombe la FA"

Simba na Yanga zote zimetinga robo fainali wakisubiri droo ya hatua hiyo ambayo itafanyika baada ya April 17

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
13h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
17h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’