Vilabu vyagomea kanuni mpya ya TFF

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
30 Mar 2020
Vilabu vyagomea kanuni mpya ya TFF

Timu za Ligi Kuu Tanzania Bara zimegomea mfumo mpya unaotarajiwa kuanzishwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wa kuhakikisha klabu zinatumia kiwango cha fedha halali kulingana na kiasi kitakachokubalika katika uendeshaji kwa msimu.

Siku chache zilizopita Rais wa TFF, Wallace Karia alikaririwa na vyombo vya habari akisema kwa sasa wanafanya mpango na utaratibu wa kuja na mfumo huo kwa timu kuanza kukagua timu zinazoshiriki ligi hiyo kama fedha halali wanazoingiza wanatumia ipasavyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, viongozi wa timu za Simba, Yanga, Azam FC na Mwadui walisema mfumo huo sio muafaka kwa sasa, kwani TFF walitakiwa kufanya mambo ya msingi kama kuandaa mazingira mazuri ya mchezo huo ili klabu ziwe na uwezo kifedha.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema TFF walipaswa kwanza kutengeneza kamati iliyojaa wadau wa mchezo huo ambayo ingekuwa maalumu kwa kufanya utafiti na uchunguzi wa muda mrefu na kuja na majibu kama mfumo huo unaweza kutumika au la.

"TFF walipaswa kwanza kutengeneza kamati ambayo ingeshirikisha wajumbe wa mchezo wa soka ambao kazi yao maalumu ingekuwa kufanya uchunguzi na utafiti kuangalia kama jambo hilo ni wakati sahihi kuanza kutumika au la"

Alisema ni mfumo mzuri ambao unatumiwa na mataifa makubwa yaliyoendelea kisoka, lakini kwa Tanzania sio wakati wake, kwani kama wataanzisha basi wategemee mchezo kutopiga hatua kimaendeleo na badala yake, timu hazitakuwa na uwezo wa kusajili wachezaji wenye uwezo kutoka nje ya nchi.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Sezo Mazingiza alisema mfumo wa ‘Financial Fair Play’ ni mzuri kwa kila mtu anayetamani kuona maendeleo ya mchezo wa soka, lakini kwa Tanzania ni mapema mno kuanza kuutumia.

Alisema TFF wanatakiwa kuweka kipaumbele kuhakikisha kila timu inayoshiriki ligi hiyo inakuwa na leseni, kuwa na maendeleao mazuri kwenye soka la vijana kwa kuwa na makocha wenye vigezo na uwezo wa kuibua vipaji na kuviendeleza.

“Mfumo wa Financial Fair Play kama wanaoutumia Ulaya ni mzuri kutokana na mazingira yao yanaruhusu na kila mtu anatamani, lakini kwa Afrika na hasa Tanzania sio muda wake, kwani walitakiwa kujikita katika mambo muhimu kwanza, “alisema.

Alisema kuna mambo mengi TFF walitakiwa kuyawekea msisitizo kwa soka la vijana kwa klabu na maendeleo ya timu za taifa, lakini hili bado.

Alisema TFF walitakiwa kuhakikisha kila klabu inakuwa na utawala bora, utaratibu mzuri wa ukaguzi wa fedha na uongozi sahihi.

Alisema wanatakiwa kuhakikisha timu zote zinakuwa na uwezo wa kifedha wa kusajili wachezaji wa kigeni wenye uwezo, kuwa na makocha wazuri wa madaraja makubwa wa ndani na hata nje ya nchi, klabu kuwa na viwanja vya uhakika vya mazoezi na mechi.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria ‘Thabit Zakazi’ alisema biashara ya mchezo wa soka la Afrika haipo, hivyo klabu nyingi zinategemea fedha kutoka nje ya vyanzo vyao vya mapato kujiendesha.

“Wenye uwezo wa kuendesha mpira kutokana na biashara ya mpira ni timu ambazo zina mashabiki wengi kwa Afrika mfano kwa Tanzania ni kama Yanga na Simba wana mashabiki wengi, lakini bao bado hawawezi kuendesha timu kwa fedha zao wenyewe, hakuna timu ambayo ina uwezkuwa hata hizo Simba na Yanga pamoja na ukongwe wao, lakini bado hawawezi kusajili wachezaji wa kulipwa kwa kutumia fedha zao, kwani hawana kipato hicho.

Alisema hata TFF wenyewe kuna wakati wanakosa fedha za kujiendesha na wanaomba msaada kwa wadau kuwasaidia akitolea mfano, Rais John Magufuli alitoa fedha kwa ajili ya timu ya Taifa Stars kwa ajili ya kucheza mchezo wa kutafuta tiketi ya kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon).

“Hata TFF hawatengenezi faida ya mchezo wa soka na ndio maana wanaomba fedha kwa wadau kusaidia timu za Taifa, “alisema.

Zakazi alisema cha msingi TFF wanatakiwa kushirikiana na klabu zote katika kila mchakato wa kuzisaidia klabu kuwa na vyanzo vyao vya fedha na kuweza kujiendesha, lakini si sasa timu hazina uwezo huo.

Katibu Mkuu wa Mwadui FC, Ramadhan Kilao alisema timu nyingi zinazoshiriki ligi zinategemea fedha kutoka kwa wafadhili ili kujiendesha lakini kuleta mfumo huo bado utakandamiza maendeleo ya timu.

“Kwa mfano sisi Mwadui usajili wetu ni Sh milioni 150 lakini kwa timu za Simba na Yanga ni zaidi ya milioni 800 hadi bilioni na bado ligi ikimalizika timu inakuwa na madeni kibao, binafsi naona TFF wanapaswa kujikita kuzisaidia timu kujimudu kifedha, “alisema Kilao.

Mchakato huo ulianza hivi karibuni kwa Bodi ya Ligi (TPLB) ilifanya ziara kutembelea timu zinazoshiriki ligi kueleza baadhi ya mahitaji wanayotakiwa kuwa nayo ili kupata leseni kuanzia msimu ujao.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’