Moja ya udhaifu anaotajwa kuwa nao mlinda lango namba moja wa Simba Aishi Manula, ni kufungwa mabao nje ya 18
Ni tatizo ambalo limekuwa likizungumzwa na mashabiki mara kwa mara na lilimgharimu kukaa nje kwa takribani mechi saba baada ya mchezo wa kwanza dhidi ya Yanga ambao ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2
Manula amezungumzia changamoto hiyo ambayo kimsingi amesema ni mtazamo wa mashabiki tu
Manula amesema mashabiki wamekuwa na kasumba ya kumuangalia yeye na mechi kubwa za Simba na Yanga ndio maana wanakuwa na maoni hayo
"Si kwamba mimi nafungwa magoli yanayofanana ila ni wadau wa soka wao kuniangalia mimi au michezo ya Simba ama Yanga tuu ndio maana hawasemei michezo mingine"
Pamoja na hivyo Manula amesema ataendelea kujiimarisha ili kuhakikisha anakuwa kwenye kiwango bora kuipa mafanikio klabu yake ya Simba
Β