Simba kesho inashuka kwenye dimba la Taifa ikiwa mwenyeji wa Singida United katika mchezo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka.
Simba inahitaji kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo ili kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi. Ushindi utaifanya iizidi Yanga iliyotoka sare na Mwadui FC kwa alama saba.
Simba iko kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na alama 26 sawa na Azam FC zikitofautiana mabao tu huku Singida United iko nafasi ya nne ikiwa na alama 23.
Habari njema kwa kikosi cha Simba ni kurejea kikosini kwa mshambuliaji Emanuel Okwi, kinara wa upachika mabao ligi kuu ya Vodacom akiwa na mabao nane.
Okwi ana rekodi nzuri ya kupachika mabao kwenye uwanja wa Taifa kwani mabao yake yote ameyafunga kwenye uwanja huo na ule wa Uhuru.

ADVERTISE HERE