Kagere ataja usajili wa Ligi ya mabingwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Mar 2020
Kagere ataja usajili wa Ligi ya mabingwa

Mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere ‘MK14’ amefunguka kuhusu usajili ambao angependa kuuona Msimbazi msimu ujao.

Kagere ambaye kwa sasa yuko Rwanda alikojiweka mwenyewe karantini na familia yake ili kujiepusha na virusi vya Corona, pia ametoa pia angalizo kwa mashabiki.

Kagere amesema kwamba Simba kwa sasa ni timu kubwa ya kimataifa na yenye wachezaji bora, hivyo watakaokuja watapaswa kuwa bora zaidi ya waliopo yaani aliyepo ndani ya uwanja akimuangalia wa benchi atokwe na jasho.

"Wachezaji wote waliopo ni bora sana, ndio maana tunafanya vizuri mpaka sasa, hivyo viongozi wetu wanahitaji kutumia akili za ziada ili hao watakaokuja wawe mafundi zaidi, yaani namba moja iwe na wataalamu zaidi ya wawili, ili kikitoka kitu kinaingia kitu zaidi,” alisema mchezaji huyo raia wa Rwanda aliyezaliwa Uganda.

“Kama tunaongeza beki, basi anahitajika kuwa na uwezo zaidi ya waliokuwapo katika timu wakati huu. Yaani atakayeingia na atakayetoka pasiwe na tofauti.

“Tukifanikiwa kuingiza wapya wenye ubora kama au zaidi ya sisi tuliopo itaongeza hali ya kushindana na kila mmoja ataongeza umakini ili kupata nafasi ya kucheza, atataka kuonyesha kiwango cha hali ya juu katika nafasi ambayo anaitumikia.

“Hii itasaidia kubadilisha ubora soka letu kwa vile ni klabu kubwa ya kimataifa, lengo letu wachezaji ni kutwaa vikombe mbalimbali zaidi ilivyo sasa, halitakuwa jambo la kupendeza kama wanasajiliwa wachezaji wapya ambao wanakuja katika timu wanaonekana tayari wamelewa mafanikio na kushindwa kutoa ushindani kwa ambao wamewakuta.”

“Hivyo ndivyo mtazamo wangu ulivyo, naona tutakuwa na kikosi bora na imara zaidi huku tuendako na mashabiki watafurahi,” aliongeza Kagere mwenye mabao 19 kwenye Ligi Kuu Bara. “Lakini jambo jingine ambalo litakuwa la kupendeza katika timu ni kuwe na wachezaji wengi wa viwango vya juu.

"Haitakiwi mchezaji fulani akikosekana katika mechi mashabiki au wachezaji wenyewe wasikitike, bali inatakiwa yeyote ambaye anakuwapo kazi ifanywe kwa ubora uleule au unaokaribiana. Huo ndio mtazamo wangu katika usajili wetu msimu huu"

“Lakini tukiweza kupata wachezaji bora nitafurahi sana, nina imani hawatakuwa wapya wengi kwani timu iko vizuri.”

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
6h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
12h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
15h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’