Mapumziko ya Corona yatatuimarisha - Wawa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Mar 2020
Mapumziko ya Corona yatatuimarisha - Wawa

Beki kisiki wa Simba Paschal Serge Wawa amesema pamoja na kuwa wako majumbani kutokana na janga la Corona, wanaendelea kufanya mazoezi binafsi na watarejea wakiwa imara

Wawa ambaye mpaka sasa amekuwa na msimu mzuri, amesema kocha Sven vandenbroeck aliwapa program ya mazoezi ambayo anaamini itawaimarisha

Beki huyo raia wa Ivory Coast amesema malengo yao ni kutetea ubingwa wanaoushikilia kwa misimu miwili, hivyo hakuna mchezaji anabweteka mpaka wahakikishe wametwaa ubingwa

"Mimi naendelea na mazoezi, wachezaji wote tulipewa program ambayo tunapaswa kuikamilisha kabla ya ligi kurejea," amesema Wawa

"Najua kila mchezaji huko aliko anafanya mazoezi kwani kama wachezaji tulijiwekea malengo kuwa tukirudi tukamilishe ligi kwa kushinda ubingwa mapema"

"Hatuwezi kubweteka kwani tunafahamu pamoja na kuwa tunaongoza kwa alama nyingi, tukizembea lolote linaweza kutokea. Mechi za mwisho mara nyingi zinakuwa na ushindani"

Mwazi Juni Wawa atakamilisha msimu wake wa pili akiwa na klabu ya Simba lakini tayari mazungumzo ya kumuongezea mkataba mpya yameanza

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
2h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
20h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’