TFF itoe wiki ya maandalizi Ligi ikirejea - Mingange

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Mar 2020
TFF itoe wiki ya maandalizi Ligi ikirejea - Mingange

Kocha mkuu wa timu ya Ndanda FC, Meja mstaafu Abdul Mingange ameliomba Shirikisho la soka Tanzania (TFF) liwape muda wa wiki moja kujiandaa ligi ikirejea kwakua ana imani wachezaji hawatakuwa fiti.

Ligi imesimama kwa mwezi mmoja kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya Corona ambavyo tayari vimeingia nchini.

Meja Mingange amesema wachezaji wengi wa Tanzania sio professional kwahiyo kipindi hiki wanaweza wakaona ni mapumziko kwahiyo ligi ikiendelea wanakuwa kama wanaanza upya hivyo wanahitaji muda kukaa sawa.

Kocha huyo ameongeza kuwa wamewapa wachezaji wao program za kufanya mazoezi nyumbani lakini kuzifuatilia huenda ikawa ngumu hivyo wakarejea wakiwa hawapo fiti.

"Ninadhani TFF itupe wiki moja ya kujiandaa ligi ikirejea maana kwa wachezaji wetu hawa watarudi wakiwa hawako fiti kwahiyo itakuwa ngumu kama wataanza ligi moja kwa moja.

"Wachezaji wangu nilisha waandaa kucheza dakika 90 lakini wakirudi huenda wasiwe fiti kucheza hata dakika 60 kwahiyo nadhani tunapaswa kupata muda wa kufanya mazoezi ya pamoja kabla ya ligi kuendelea," alisema Meja Mingange

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
43m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’