Fraga afurahia maisha Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Mar 2020
Fraga afurahia maisha Simba

Kiungo wa Simba raia wa Barazil Gerson Fraga, amesema ana furaha kuwatumikia mabingwa hao wa nchi akiwa na imani kuwa ataendelea kubaki Msimbazi

Mkataba wa Fraga unaelekea ukingoni, alitua Simba mwanzoni mwa msimu akitokea nchini India

Fraga amesema anajisikia faraja kucheza kwenye kikosi cha Simba ambacho kimesheheni nyota wengi wenye vipaji

Amewataja wachezaji wanaomvutia zaidi ni pamoja na Francis Kahata, Hassan Dilunga, Meddie Kagere, Miraji Athumani na Deo Kanda.

"Deo Kanda napenda zile chenga zake za maudhi, kama anakwenda huku anarudi.. Namkosa sana Miraji, nilimuuliza lini unakuja, akasema karibuni," alisema kwa Kiswahili chake cha kubabaisha.

Katika mahojiano ya mtandaoni na mashabiki wa Simba juzi, Fraga alibainisha kuwa chakula anachokipenda mno Tanzania ni makange, nyama ya mbuzi na ugali, akidai kuwa akipata chakula hicho na chupa ya maji siku yake inakuwa nzuri mno, tofauti na vyakula vingine.

Mechi yake kubwa anayoikumbuka ya Ligi Kuu ni ile ambayo Simba ilicheza dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

Kwenye mechi hiyo Fraga alifunga mabao yote mawili ya ushindi, Simba ikiitandika Coastal 2-0 kwenye Uwanja wa Uhuru Februari Mosi, mwaka huu.

Hata hivyo, amesema bao lake bora ni lile alilolifunga kwenye mechi dhidi ya KMC katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, Desemba 28, mwaka jana alipofunga dakika za nyongeza, Simba ikishinda mabao 2-0, baada ya Kanda kuitanguliza mbele

Mpaka sasa Fraga ana mabao matatu kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, ingawa kwa siku za karibuni amekuwa hapati sana nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
11h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
14h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’