Simba yamkomalia Mwamnyeto

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 Mar 2020
Simba yamkomalia Mwamnyeto

Baada ya kumkosa kwenye dirisha dogo, klabu ya Simba inaelekea itafanikiwa kumnasa beki kisiki wa Coastal Union Bakari Nondo Mwamnyeto ambaye pia yuko timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'

Inaelezwa mazungumzo ya kumsajili nyota huyo yalifanyika tangu mwaka jana lakini changamoto iliyokuwepo ni dau kubwa la usajili ambalo klabu ya Coastal Union ilitaka

Coastal Union ilikuwa tayari kumuuza Mwanyeto kwa Tsh Milioni 80 dau ambalo walilipandisha baada ya Simba na Yanga zote kugongana zikimuwania mlinzi huyo chipukizi

Lakini inaelezwa mkataba wake na Coastal Union umebaki mwaka mmoja na mazungumzo mapya yamefanyika, mabosi wa Simba wakiwa tayari kutoa kiasi hicho cha fedha waweze kumsajili

Aidha zipo taarifa kuwa nyota huyo ameandaliwa mkataba wa miaka mitatu

Simba inatarajiwa kuongeza nguvu safu yake ya ulinzi ili kuhakikisha inakuwa imara kuelekea michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu ujao

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’