Ule mchakato wa kuwaongezea mikataba ibaadhi ya wachezaji wa Simba unaendelea ambapo wakati wowote beki Paschal Wawa na viungo Sharaff Shiboub na Mzamiru Yassin wanatarajiwa kusaini mikataba mipya kuendelea kubaki Msimbazi
Shiboub alitua Simba mwanzoni mwa msimu kwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja, kocha Sven Vandenbroeck amependekeza aongezwe mkataba akiungana na Mzamiru ambaye mkataba wake wa awali wa miaka mitatu unamalizika mwezi Juni
Beki kisiki Paschal Wawa yeye anaongezewa mkataba baada ya kuonyesha ubora msimu huu
Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amesema watahakikisha wanawapa mikataba mapema nyota wote ambao wanawahitaji kuendelea kubaki nao ili kuondokana na usumbufu unaojitokeza wakati wa dirisha la usajili
ADVERTISE HERE