Wachezaji wa Simba watalazimika kusubiri siku 30 zilizotolewa na Serikali kuweza kurejea mazoezini kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona
Awali uongozi wa Simba uliwapa wachezaji mapumziko ya siku saba huku wakisubiri maelekezo mengine kutoka kwa uongozi
Hata hivyo kutokana na hatua zinazoendelea kuchukuliwa kujikinga na janga hilo, ni wazi watalazimika kusubiri kwa siku 30 kabla ya kurejea kikosini
Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema mapumziko hayo yatakuwa na faida kwa wachezaji wake kwani anaamini watarejea wakiwa na ari na nguvu ya kumaliza msimu kibabe
Simba inahitaji kushinda mechi tano kati ya 10 zilizobaki ili kujihakikishia ubingwa wa tatu mfululizo
ADVERTISE HERE