Maboresho ambayo kila Mwanasimba angependa kuyaona

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 Mar 2020
Maboresho ambayo kila Mwanasimba angependa kuyaona

Wadau mbalimbali wa klabu ya Simba wametoa maoni yao kuhusu maboresho ya usajili ambayo wangependa kuyaona kipindi cha usajil kinachokuja

Wakati ligi ikiwa imesimama kutokana na janga la ugonjwa wa Corona, kimahesabu Simba ina nafasi kubwa zaidi ya kutetea ubingwa wake kwa msimu wa tatu mfululizo

Hivyo mabingwa hao wa nchi msimu ujao watakuwa na jukumu la kuibeba Tanzania kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Mwaka juzi Simba ilifanikiwa kutinga robo fainali ya michuano hiyo na kuisaidia Tanzania kupata nafasi nne za uwakilishi kwenye michuano hiyo

Lakini msimu uliopita pasipo na matarajio ya wengi, Simba iliondoshwa katika hatua za awali

Ili kuhakikisha timu inafanya vizuri msimu ujao, kwa maoni ya wengi, kuna haja ya kufanyika maboresho kwenye baadhi ya maeneo

1. Beki wa kati

Pamoja na wakongwe Paschal Wawa na Erasto Nyoni kuweza kuhimili mikiki mikiki ya Ligi Kuu, wengi wanaona Simba inahitaji kusajili walinzi wengine wenye uzoefu wa mechi za Kimataifa ambao watasaidiana nao

Mabeki hao umri umewatupa mkono na wamekuwa wakisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara

Walinzi wengine ukiondoa wao hawafikii ubora wa kuihakikishia Simba kufanya vizuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa

2. Mlinzi wa kulia

Shomari kapombe ndiye anayetegemewa zaidi kwa sasa baada ya Haruna Shamte kushindwa kuonyesha makali yake

Wadau wanaamini nafasi hii inapaswa kuongezewa nguvu

3. Mshambuliaji

John Bocco na Meddie Kagere bado wanao uwezo wa kuibeba Simba kwenye michuano ya Kimataifa. Lakini changamoto yao haina tofauti na ya Wawa na Nyoni

Hofu kubwa ni pale inapotokea mshambuliaji mmoja au wote wakipata majeraha. Nje Simba haina mshambuliaji wa aina yao ambao anaweza kuchukua nafasi wanapokosekana

Msimu huu Bocco alikaa nje kwa muda mrefu kutokana na majeraha. Kuna wakati kukosekana kwake kuliipa changamoto safu ya ushambuliaji ya Simba kwani Kagere aliachiwa mzigo mkubwa peke yake

Hili ni eneo ambalo wanasimba wengi wamependekeza liongezwe nguvu

Smba kusajili nyota watano

Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amefunguka kuwa wameshapokea mapendekezo ya kocha Sven Vandenbroeck kuhusu usajili

Wanatarajia kusajili wachezaji wapya watano ambapo usajili huo utazingatia kwa kiasi kikubwa maoni ya wadau

"Kocha ametupa mapendekezo yake, anataka mabeki watatu, kiungo na mshambuliaji. Tutakuwa makini kuhakikisha tunapata wachezaji ambao watakuwa na hadhi ya kuitumikia timu yetu"

"Mwezi Januari tumeanza na Miquissone, Wanasimba wawe na subira kila kitu kitakwenda sawa"

Simba tayari imelitawala soka la Tanzania hivyo mashabiki kwa sasa wanataka kuona mabingwa hao wa nchi wakichomoza kwenye anga za Kimataifa kwa kula sahani moja na vigogo kama Al Ahly, TP Mazembe, Zamaleki, Esperance, Mamelodi Sundows, Wyday Athletic n.k

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’