Miquissone kujenga ufalme wake Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
25 Mar 2020
Miquissone kujenga ufalme wake Simba

Kiungo mshambuliaji wa Simba Luis Miquissone amesema mabao matatu aliyofunga mpaka sasa ni mwanzo tu wa safari ya mafanikio ambayo anataka kuitengeneza pale Msimbazi

Miquissone amesajiliwa na Simba dirisha dogo akitokea klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ambayo hata hivyo ilikuwa imemtoa kwa mkopo UD Songo ya Msumbiji

Licha ya kuanza taratibu maisha yake ya soka nchini, kwa sasa Miquissone ni mchezaji tegemeo kwenye kikosi cha kwanza cha mabingwa hao wa nchi

Mwenyewe amesema hakuwa na mwanzo mzuri kwa kuwa alijiunga na Simba wakati akiwa likizo baada ya Ligi Kuu ya Msumbiji kumalizika

"Nilikuja hapa nikitoka likizo kule Msumbiji ligi ilikuwa imemalizika. Nashukuru baada ya kufanya mazoezi na timu nimeanza kuimarika ingawa bado sijafika pale nitapotaka, " amesema

"Malengo yangu ni kuisaidia Simba kwa kuifungia mabao mengi. Nimefunga mabao matatu lakini naona nina nafasi ya kufunga mabao mengi mechi zilizobaki kumaliza msimu"

Miquissone amejipambanua kwa kuwa mchezaji wa aina yake

Ana kasi, nguvu na silaha yake kubwa zaidi ni uwezo wake wa kutumia miguu yote miwili kwa ufasaha

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
10h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
14h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’