Mkakati wa usajili Simba uko namna hii

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Mar 2020
Mkakati wa usajili Simba uko namna hii

Kama mikakati ya Simba ikienda sawa huenda wakamaliza usajili kabla ya msimu huu wa Ligi Kuu Bara haujamalizika na kuweka historia ya aina yake.

Tayari Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amedokeza kuwa wamepokea ripoti ya awali kutoka kwa kocha, Sven Vendenbroeck inayohitaji mastaa watano wa maana.

Senzo amebainisha kwamba jambo la kwanza Kocha anataka wachezaji wasizidi watano tu na wao kama uongozi wamempa nafasi ya kutaja wachezaji ambao anawataka ili kuona kama wana uwezo kuwasajili.

Senzo anasema amewaambia anataka mastraika wawili, kiungo mwenye uwezo wa kucheza kwenye kukaba na kushambulia pamoja na beki wa kati lakini na Wabongo kadhaa.

Anasema wao uongozi wamempa nafasi hiyo mapema Sven kutaja wachezaji ambao anawataka ili kupunguza presha ya usajili pindi dirisha litakapofunguliwa na si kama kila mchezaji ambaye atakuwa amependekeza atasajiliwa kwani katika kila eneo moja ambalo anataka kutakuwa na wachezaji watatu chaguo la kwanza.

"Katika hili la usajili tumeanza tayari skauti katika maeneo mengi hapa Afrika ili kupata wachezaji bora na imara pengine tutafanya usajili mzuri kuliko misimu yote kwani kuna vigezo vingi kulingana na mahitaji yetu. Hatutasajili kwa mihemko," Mazingisa aliiambia Mwanaspoti

"Jambo la pili, Sven amependekeza kutoa ruhusa kwa wachezaji wale ambao hawakuwa wanapata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenda katika timu nyingine hata kama wakiwa bado wana mikataba au wamemaliza

"Suala la tatu ambalo Sven aliweka katika ripoti yake ni kwamba skauti ifanyike kwa kutumia kampuni ambazo zinaweza kumuangalia mchezaji na kumuelezea ubora na udhaifu wake, zoezi hilo lilifanyika kwenye usajili wa msimu uliopita tukitumia moja ya kampuni za Afrika Kusini.

"Jambo la nne, Sven amewataka wachezaji wake huko walipo wajilinde na Corona pamoja na kufanya mazoezi peke yao, lakini kuweka miili yao sawa ili kumalizia vizuri mechi zilizobaki na kukamilisha malengo yao ya kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu,” alisema Senzo.

"Suala la mwisho tumeanza kuangalia wachezaji katika ligi ya ndani ambapo tunaweza kusajili hata wawili na maeneo mengine Afrika katika nchi ambazo zimeendelea kisoka,” alisisitiza Senzo"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’