Beki mkongwe ndani ya Klabu ya Simba, Erasto Nyoni amesema kuwa atajumuika na wachezaji wenzake kwenye mazoezi ya pamoja baada ya mapumziko ya mwezi mmoja kukamilika.
Nyoni alipata majeraha kwenye mchezo dhidi Yanga uliopigwa Uwanja wa Taifa Machi 8 ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kwa muda ili kukabiliana na changamoto ya maambukizi ya virusi vya Corona
"Ninaamini baada ya muda wa mwezi mmoja nitakuwa sawa, nitaungana na wenzangu kwenye mazoezi, kikubwa ni kuomba Mungu tuwe salama kwani hili janga ni hatari" amesema Nyoni
ADVERTISE HERE