Mwekezaji Simba hadharani Jumamosi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
7 Oct 2017
Mwekezaji Simba hadharani Jumamosi
Kamati Maalum ya kusimamia mchakato wa zabuni ya kumpata mwekezaji kwenye muundo mpya wa klabu ya Simba kesho Saa 5:00 asubuhi inatarajiwa kukutana na Waandishi wa Habari.

Tarifa ya Simba SC kwa vyombo vya Habari vya Habari iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu, Hajji Sunday Manara imesema kwamba mkutano huo utafanyika kwenye ukumbi wa Kivukoni 3 uliopo ndani ya hoteli ya Serena mjini Dar es Salaam.

Kamati hiyo iliyoundwa mapema mwezi uliopita, ipo chini ya Mwenyekitil, Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu Thomas Mihayo na Wajumbe wengine wanne, ambao ni Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan ‘Zungu’, Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Abdul-Razaq Badru, Wakili Dk. Damas Ndumbaro na Yusuph Maggid Nassor.

Ikumbukwe Agosti 20, mwaka huu wanachama 1,216 wa klabu ya Simba waliridhia mfumo wa klabu yao kuuza Hisa baada ya Mkutano uliofanyika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere (MNICC), Dar es Salaam.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na Waziri wa Afya Jinsia na Watoto, Dk Hamisi Kigwangala, Kaimu Mwenyekiti wa klabu, Salim Abdallah 'Try Again' alisema kwamba asilimia 50 ya hisa zitauzwa kwa mwekezaji yeyote au wowote watakaoungana wasiozidi watatu, kwa sharti moja tu la kuwa wanachama wa klabu hiyo.

Abdallah alisema mwekezaji huyo au hao, wanatakiwa kuweka dau lisilopungua Sh. Bilioni 20 ili kupatiwa asilimia 50 ya hisa za klabu, wakati kwa kuanzia wanachama wote wa Simba wamepewa asilimia 10 ya hisa.

Alisema asilimia nyingine 40 zitawekwa kama mtaji wa klabu na zitauzwa kwa wanachama baadaye, lakini wale wawekezaji walionunua asilimia 50 awali, hawataruhusiwa kununua hata hisa moja kwenye asilimia 40 za mtaji.

Na baada ya mkutano wa huo, zoezi la uhakiki wa wanachama wa ili kujua mgawanyo wa asilimia 10 za hisa utakavyokuwa – lilifuatia kabla ya kuundwa Kamati maalum ya kupitia maombi ya wawekezaji wanaotaka kununua asilimia 50 ya hisa.

Kadhalika Simba iliendesha mikutano maalum katika mikoa kadhaa nchini kuwapa elimu ya mabadiliko wanachama wake.

Na mfanyabiashara na mfadhili wa zamani wa klabu hiyo, Mohammed ‘Mo’ Dewji ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kununua asilimia 50 ya hisa Simba.

Tangu mwaka jana, Mo Dewji amekuwa akiisaidia uendeshwaji wa Simba kwa matarajio ya ndiye atakayepewa umiliki wa klabu katika mfumo mpya.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1m ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE →