Kakolanya kuendelea kumkomalia Manula Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 Mar 2020
Kakolanya kuendelea kumkomalia Manula Simba

Mlinda lango wa Simba, Beno Kakolanya, amesema ataendelea kukitumikia kikosi hicho, licha ya kukosa namba ya kudumu kutokana na ushindani.

Kauli hiyo ni kama salamu kwa mpinzani wake Aishi Manula kuwa asibweteke akifahamu mwenzake huyo yupo katika hesabu kali jinsi ya kupata nafasi Msimbazi na si kutimka. 

Kakolanya amekuwa akitumika kama kipa namba mbili katika kikosi cha Simba, nyuma ya Manula.

Kakolanya aliyetua Simba baada ya kuvunja mkataba wake na Yanga, amesema bado ana nafasi kubwa ya kuitumikia timu yake, licha ya ushindani anaoupata kutoka kwa Manula.

"Ni kawaida kwa kocha kumpa nafasi mchezaji anayemuona yupo vizuri, silaumu Manula kupangwa, naamini hata mimi nina nafasi, siku yangu haijafika, kama ikifika hakuna kitakachozuia," Kakolanya amenukuliwa na gazeti la Bingwa

"Binafsi naumia kuona nimeisaidia timu yangu michezo michache katika ligi, lakini bado ipo mingine niliyokaa langoni kama mechi za Mapinduzi, pamoja na FA, hivyo inawezekana Manula akatumika katika ligi na mimi nikapata nafasi kwenye mashindano mengine, kikubwa wote tunaisaidia Simba ishinde tu"

Kipa huyo amedaka michezo saba ya Ligi Kuu Bara kati ya 28, ambayo Simba imecheza.

Kwa sasa Simba inaongoza katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi 71, baada ya kucheza michezo 28, sawa na Azam wanaoshika nafasi ya pili kwa pointi 54.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’