Tairone, Fraga waitega Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 Mar 2020
Tairone, Fraga waitega Simba

Nyota wawili raia wa Brazil Tyrone Da Silva na Gerson Fraga wako ukingoni mwa mikataba yao waliyosaini mwaka jana

Nyota hao kila mmoja alisaini mkataba wa mwaka mmoja na mpaka kufikia mwezi Juni watakuwa wachezaji huru

Tayari tetesi zimezagaa kuwa hawatakuwa sehemu ya kikosi cha Simba msimu ujao kwani hawatapewa mikataba mipya

Ukifanya tathmini ya kawaida kabisa utaweza kukubali kuwa Fraga ameonyesha kiwango cha kuridhisha katika mechi nyingi alizopata nafasi

Anaweza asiwe mchezaji bora sana lakini ana vitu vingi vinavyoweza kuisaidia timu pale inapokuwa imekwama

Rejea magoli yake mawili kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union

Ni mchezaji mwenye juhudi, jasiri na anaweza kucheza soka la aina zote, kistaarabu au kibabe

Kwa Fraga pengine Simba itahitaji kupitia uamuzi wake mara mbili kabla ya kuamua kumnyima mkataba

Upande wa Tairone, nadhani hataongezewa mkataba, hilo liko wazi. Ni mchezaji mzuri lakini nadhani Simba inahitaji ubora zaidi yake

Nyota mwingine Wilker Da Silva aliondoka mapema tu mwezi January

Nadhani huyu alipata bahati tu ya kusajiliwa Simba, lakini hakuwa mchezaji mwenye maajabu

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
48m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’