Leo Rais wa TFF Wallace Karia ametoa tamko kuwa wachezaji na wafanyakazi wa kigeni waliosafiri kurudi makwao, hawataruhusiwa kurejea nchini kutokana na mlipuko wa ugonjwa Corona
Karia alikwenda mbali zaidi kwa kusema wachezaji hao pia watakaporejea hawataruhusiwa kushiriki ligi
Tamko hilo limepokewa kwa mshangao na wadau wengi wa soka nchini kwani bado Serikali haijazuia watu kusafiri
Lakini pia Serikali haijafunga mipaka kuzuia wageni kuingia hivyo tamko hilo ni kama limetolewa wakati usio wake
Serikali imechukua hatua njema kuzuia michezo kwa muda wa siku 30 lakini bado haijaona kwa sasa kama kuna ulazima wa kuzuia wageni kuingia nchini, huo sio wajibu wa TFF
Jana Simba ilimruhusu mshambuliaji wake Meddie Kagere kurejea kwao Rwanda kumuona mama yake mzazi ambaye ni mgonjwa
Hili jambo la dharura na bila shaka nyota huyo alichukua tahadhari zote kabla ya kuondoka na hakuna shaka atafanya hivyo wakati atakapokuwa akirejea
Kama hatakuwa na tatizo lolote atakaporejea na Serikali ikiwa haijafunga mipaka, TFF haitakuwa na sababu ya kumzuia asicheze