Sven anaamini mapumziko yatawaimarisha wachezaji wake

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 Mar 2020
Sven anaamini mapumziko yatawaimarisha wachezaji wake

Mkufunzi wa Simba Sven Vandenbroeck amesema mapumziko waliopewa wachezaji kutokana na janga la Corona, yatawafanya warejee wakiwa na nvguvu zaidi

Juzi Simba ilitoa mapumziko ya siku saba kwa nyota wake wa kikosi cha kwanza huku kukiwa na uwezekano muda huo kuongezwa baada ya Serikali kuzuia shughuli zote za michezo zenye mikusanyiko kwa muda wa siku 30

Sven amesema kucheza mfululizo ni changamoto iliyokuwa ikimuumiza kichwa kwani alifahamu wachezaji wake walikuwa wamechoka

"Baadhi ya wachezaji walikuwa wananiambia wamechoka kutokana na kucheza mechi mfululizo lakini kwa sasa watapata muda wa kupumzika na kurejea kwenye ubora wao," amesema Sven

"Ninaamini itakuwa bora kwetu na nafuu na itaongeza umakini katika kujihakikishia ubingwa ambao tunakaribia kuupata"

Baada ya mapumzo, ligi itakaporejea mchezo wa kwanza Simba itacheza na Ruvu Shooting

Katika michezo 10 iliyobaki, Simba inahitaji kushinda michezo mitano tu ili kujihakikishia ubingwa wa tatu mfululizo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
11h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’