Wawa ajihakikishia mkataba mpya Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
20 Mar 2020
Wawa ajihakikishia mkataba mpya Simba

Kiwango kilichoonyeshwa na beki mkongwe Paschal Wawa kwenye mechi za hivi karibuni, kimewashawishi mabosi wa Simba kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja

Kwa sasa Wawa ndiye kiongozi wa safu ya ulinzi ya Simba, anatarajiwa kusaini mkataba mpya wakati wowote

Msimu huu Simba imepanga kuhuisha mapema mikataba ya nyota wake ili dirisha la usajili litakapofunguliwa wajikite katika kusaka nyota wapya

Nyota wengine ambao watasaini mikataba mipya ni pamoja na Mzamiru Yassin na Sharaff Shiboub

Taarifa za uhakika ni kuwa Simba imepanga kuongeza walinzi wawili wa kati pamoja na mlinzi wa kulia

Nyota hadi sita wanaweza kusajiliwa dirisha kubwa ambapo nafasi ya mshambuliaji mmoja pia imepewa kipaumbele

Pia viungo wawili wanaweza kutua, mmoja akiwa kiungo mkabaji

Usajili huo huenda ukawaweka matatani Tairone Da Silva na Gerson Fraga ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu

Nyota wengine ambao wanaweza wakakosa mikataba mipya ni pamoja na kiungo Said Ndemla, Yusufu Mlipili, Haruna Shamte na Shiza Kichuya aliyetua kwa mkopo usajili wa dirisha dogo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
4h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’