Kiungo fundi wa Simba Jonas Mkude amevunja ukimya baada ya anayedaiwa kuwa wakala wake Juma Ndambile kudai kuwa nyota huyo hana mpango wa kuitumikia tena timu ya Taifa kutokana na mvutano uliopo kati yake na TFF
Aidha Mkude amesema kuwa hana mpango wa kuacha kuitumikia timu ya Taifa lakini atakutana na kocha mkuu wa Taifa Stars, Etienne Ndayiragije, ili kumueleza tatizo lililomfanya ashindwe kuripoti kambini
Kuhusu alichosema Ndambile, Mkude amesema wakala wake ni Muingereza Paul Metchell, hivyo hakuna ukweli wowote katika maelezo yaliyotolewa na Ndambile
ADVERTISE HERE