Vilabu mbalimbali vinavyoshiriki ligi kuu vimevunja kambi na kuwaruhusu wachezaji kurudi makwao kufuatia tamko la Serikali kusitisha shughuli za michezo kwa muda wa siku 30 kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona ambao tayari umeingia nchini
Jana klabu za Azam Fc, Polisi Tanzania na Yanga zilitangaza kuvunja kambi zao na kuwaruhusu wachezaji kurudi makwao
Ni uamuzi ambao umechukuliwa na vilabu vingi kote duniani katika jitihada za kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona
Aidha uongozi wa klabu ya Simba ulikuwa na kikao jana ambapo pamoja na mambo mengine, huenda uamuzi wa kuvunja kambi unatarajiwa kuchukuliwa
Vinara hao wa ligi kuu wamebakisha mechi 10 na wanahitaji kushinda mechi tano tu ili kujihakikishia ubingwa wa tatu mfululizo
Kocha Mkuu wa Simba Sven vandenbroeck amesema anaamini timu itarejea na makali yake wakati ligi itakapoanza tena kutimua vumba hatua za lala salama mwezi ujao