Bodi ya Ligi yaja na Maazimio manne

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Mar 2020
Bodi ya Ligi yaja na Maazimio manne

Bodi ya ligi kuu imetangaza kuunga mkono uamuzi wa Serikali kusitisha shughuli zote za michezo kwa mwezi mmoja ili kudhibiti maambukizi ya visusi vya Corona

Katika kikao kilichofanyika leo, Bodi imeazimia mambo kadhaa ili kuhakikisha baada ya muda uliowekwa na Serikali kupita, Ligi inaendelea katika mazingira salama

Bodi imeweka maazimio manne ikiwamo ligi kuchezwa bila mashabiki baada ya siku 30 za kusimamishwa kwa mashindano yote nchini.

Ofisa Mtendaji wa Bodi (CEO), Almas Kasongo amesema katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Corona ulioingia nchini, wameazimia Ligi kuchezwa bila mashabiki itakapoendelea mwezi ujao.

"Tumeweka maazimio manne, Serikali ikijiridhisha hali ni shwari nchini na kuruhusu Ligi kuendelea, basi wachezaji wote watapimwa kabla ya mechi," alisema.

Aidha, Bodi imeazimia kuwa ligi imalizike ndani ya mwezi Juni ili kutoa nafasi kwa timu zitakazoiwakilisha nchi kimataifa kuendelea na mchakato wa mashindano ya CAF.

Lakini pia Bodi itaendelea kusimamia afya kipindi hiki cha tahadhari ya Corona

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’